Katika hotuba ya kuhitimisha bajeti hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa hotuba na moja ya jambo lililowekewa msisitizo ni hii ishu ya kupanda bei kwa bidhaa ya sukari, Waziri Majaliwa hajalikalia kimya na kusema>>’
Ni kweli kwamba uzalishaji wa sukari nchini upo chini ya kiwango cha mahitaji, mahitaji ya sukari ni tani laki 4 na 20 na kiwango cha uzalishaji ni tani laki 3 na 20 hivyo tunaupungufu wa tani laki moja‘ –Waziri Mkuu Majaliwa
‘Sukari iliyokuwepo kwenye maghala yetu imepungua, lakini tumeshaagiza na ni ile tu ambayo imepungua, hivyo wananchi watambue sukari itaingia muda si mrefu kwa ajili ya mahitaji ya kitaifa‘ – Waziri Mkuu Majaliwa
‘Natoa maagizo kwa maafisa biashara wote wafanye ufuatiliaji kwenye maduka kuona kuwa sukari haifichwi na kuuzwa kwa bei ya juu, ni matumaini yangu kuwa Watanzania watanunua sukari ileile kwa bei elekezi‘ –Waziri Mkuu Majaliwa
ULIIKOSA RIPOTI YA TUHUMA ZA RUSHWA TANZANIA NA MENGINE YA WAZIRI MKUU AKIWASILISHA BAJETI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI..
0 comments