Open top menu
Thursday 9 June 2016
Ni bajeti ya "HAPA KODI TUU"

Ikiwa ni bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya utawala wa rais John Joseph Pombe Magufuli wasomi na wataalamu mbalimbali wa masala ya uchumi nchini wameonekana kuikosoa bajeti hiyo
bajeti hiyo iliyowasilishwa Juni 8 na Waziri wa Fedha Nchini Dkt. Philip Mpango imeonekana kuwakandamizi kwa masikini kinyume na vile ambavyo serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikijinasibu
Abdul Shabani ni mtaalamu wa maswala ya uchumi ambapo yeye kwa upande wake anaimulika Bajeti hii kama ni kumnyonga mlala hoi "huwezi weka tozo ya asilimia 10 kwa miamala ya pesa kwa njia ya simu, huo ni unyonyaji" alinukuliwa Abdul
Pia alisisitiza kinyume na Matarajio ya wengi bajeti hiyo imejikita katika kuikusanyia Fedha serikali na wala sio kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini hivyo basi kuwataka wabunge kutokuipitisha bajeti hiyo
kwa upande wake Jacob Alfred ambaye yeye Mfanyabiashara wa Gesi ameeleza kusikitishwa kwake na Bajeti hiyo kutokana na kile alichokieleza kuwa bajeti hiyo ina lengo la kuwafanya Watanzania kurudi kutumia Mkaa kwa wingi
"Wanatudanganya kuwa wanataka kuimarisha matumizi ya nishati mbadala, na kumfanya kila mtanzania aweze kutumia Gesi kama nishati mbadala lakini leo wamepandisha kodi katika gesi asilia, nimesikiliza majirani zetu Kenya wao wameshusha kodi kwa gesi asilia" alikaririwa Jacob
Bajeti ya Mwaka wa fedha 2016/2017 inakadiriwa kuwa shilingi Trilioni 29.5 huku kipaumbele kikubwa katika bajeti hiyo ikiwa ni ukusanyaji wa mapato kutoka kwa wananchi
Read more
Tuesday 7 June 2016
no image

CHUO CHA MUSOMA UTALII KINAKUTANGAZIA NAFASI ZA MASOMO
Read more
no image

Mimi ni moja wa wanachuo katika chuo hiki cha Musoma utalii Tawi la Tabora,vilevile ni msomaji na mfuatiliaji mzuri sana wa gazeti lenu napenda sana jinsi mnavyotuelimisha,kutuburudisha na kufichua maovu katika chuo na jamii nzima kwa ujumla.Habari zenu zinanivutia sana kwani napenda kufahamu mambo mbalimbali yanayojitokeza katika chuo na jamii vipengele vinavyonivutia ni Makala na Kurunzi la Mwandishi.
Ninapendezwa sana na Ujasiri mnaouonesha  wa Uandishi katika Habari Zenu,mnaonesha jinsi  mnavyowajibika nakuonesha umahiri wenu katika chuo hiki na si mimi tu! Mnawavutia wengi na baadhi yao wanatamani hata kubadirisha kozi mmekuwa mfano wa kuingwa.Naomba muendelee na uwajibikaji wenu mtafanikiwa sana na mtaweza kushindana katika soko la Ajira Natumaini mtakuwa waandishi wazuri wa habari ambazo zitakazowatetea wanyonge.
Kikubwa ninachopenda kuwashauri katika  Gazeti  lenu la Umoja ni mjitahidi kuboresha Habari Zenu ziwe na ukweli katika Uwandishi na msipende kuegemea upande mmoja ambapo itapelekea habari zenu kuwa na Usawa Mzidishe ubunifu zaidi na zaidi.Pia mjitahidi kulipanua Gazeti lenu lisiwe tu na wasomaji katika chuo chetu pekee.Liweze kusambaa na Mikoa mingine hii itapelekea waandishi wenu kujulikana kwa waandishi wa kimataifa.

Mungu awabariki muendelee kuwajibika zaidi katika fani yenu najua mnakutana na changamoto nyingi katika Harakati za kutupatia habari ambazo zitatujenga msichoke kupambana kwani tunawategemea sana.
Read more

Followers