Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya stori kubwa ni hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Magufuli kujaza vijana Serikalini‘
Gazeti hili limeripoti kuwa Magufuli amesema kuanzia sasa wateule wengi
wa Serikali watakuwa vijana kwa kuwa amegundua wengi hawapendi rushwa.
Gazeti
hilo limeongeza kauli ya Rais Magufuli kuwa anafahamu kwamba vijana
hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka
Taifa katika maendeleo anayoyatamani kwani aliowaweka tayari ameshaanza
kuona matunda ya kazi zao.
Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa makandarasi wa mikoa ya Dar es salaa, Mbeya na Dodoma.
0 comments