Ikiwa ni bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya utawala wa rais John Joseph Pombe Magufuli wasomi na wataalamu mbalimbali wa masala ya uchumi nchini wameonekana kuikosoa bajeti hiyo
bajeti hiyo iliyowasilishwa Juni 8 na Waziri wa Fedha Nchini Dkt. Philip Mpango imeonekana kuwakandamizi kwa masikini kinyume na vile ambavyo serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikijinasibu
Abdul Shabani ni mtaalamu wa maswala ya uchumi ambapo yeye kwa upande wake anaimulika Bajeti hii kama ni kumnyonga mlala hoi "huwezi weka tozo ya asilimia 10 kwa miamala ya pesa kwa njia ya simu, huo ni unyonyaji" alinukuliwa Abdul
Pia alisisitiza kinyume na Matarajio ya wengi bajeti hiyo imejikita katika kuikusanyia Fedha serikali na wala sio kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini hivyo basi kuwataka wabunge kutokuipitisha bajeti hiyo
kwa upande wake Jacob Alfred ambaye yeye Mfanyabiashara wa Gesi ameeleza kusikitishwa kwake na Bajeti hiyo kutokana na kile alichokieleza kuwa bajeti hiyo ina lengo la kuwafanya Watanzania kurudi kutumia Mkaa kwa wingi
"Wanatudanganya kuwa wanataka kuimarisha matumizi ya nishati mbadala, na kumfanya kila mtanzania aweze kutumia Gesi kama nishati mbadala lakini leo wamepandisha kodi katika gesi asilia, nimesikiliza majirani zetu Kenya wao wameshusha kodi kwa gesi asilia" alikaririwa Jacob
Bajeti ya Mwaka wa fedha 2016/2017 inakadiriwa kuwa shilingi Trilioni 29.5 huku kipaumbele kikubwa katika bajeti hiyo ikiwa ni ukusanyaji wa mapato kutoka kwa wananchi

0 comments