Mimi ni moja wa wanachuo katika chuo hiki cha Musoma utalii
Tawi la Tabora,vilevile ni msomaji na mfuatiliaji mzuri sana wa gazeti lenu
napenda sana jinsi mnavyotuelimisha,kutuburudisha na kufichua maovu katika chuo
na jamii nzima kwa ujumla.Habari zenu zinanivutia sana kwani napenda kufahamu
mambo mbalimbali yanayojitokeza katika chuo na jamii vipengele vinavyonivutia
ni Makala na Kurunzi la Mwandishi.
Ninapendezwa sana na Ujasiri mnaouonesha wa Uandishi katika Habari Zenu,mnaonesha
jinsi mnavyowajibika nakuonesha umahiri
wenu katika chuo hiki na si mimi tu! Mnawavutia wengi na baadhi yao wanatamani
hata kubadirisha kozi mmekuwa mfano wa kuingwa.Naomba muendelee na uwajibikaji
wenu mtafanikiwa sana na mtaweza kushindana katika soko la Ajira Natumaini mtakuwa
waandishi wazuri wa habari ambazo zitakazowatetea wanyonge.
Kikubwa ninachopenda kuwashauri katika Gazeti
lenu la Umoja ni mjitahidi kuboresha Habari Zenu ziwe na ukweli katika
Uwandishi na msipende kuegemea upande mmoja ambapo itapelekea habari zenu kuwa
na Usawa Mzidishe ubunifu zaidi na zaidi.Pia mjitahidi kulipanua Gazeti lenu
lisiwe tu na wasomaji katika chuo chetu pekee.Liweze kusambaa na Mikoa mingine
hii itapelekea waandishi wenu kujulikana kwa waandishi wa kimataifa.
Mungu awabariki muendelee kuwajibika zaidi katika fani yenu
najua mnakutana na changamoto nyingi katika Harakati za kutupatia habari ambazo
zitatujenga msichoke kupambana kwani tunawategemea sana.
0 comments