Uongozi wa Man United leo May 27 2016 umetangaza rasmi kumpa mkataba wa miaka mitatu, kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho wenye kipengele cha kubaki katika klabu hiyo hadi mwaka 2020.
Jose Mourinho
ametangazwa na klabu hiyo lakini atajiunga na kuanza kufanya kazi rasmi
msimu wa mwaka 2016/2017 hii ina maana tutaanza kumuona Mourinho akiiongoza Man United kama kocha mkuu wakati wa mechi za maandalizi ya mechi za msimu.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho alifukuzwa kazi na Chelsea December 2015, kocha huyo mwenye asili ya Ureno toka mwaka 2003 hadi sasa akiwa kama kocha amefanikiwa kushinda jumla ya Makombe 23 katika nchi 4 tofauti.
0 comments