May 20 2016 Tanzania
imeamka na habari nyingine njema za Diamond Platnumz kuchaguliwa tena
kushiriki kwenye tuzo za kituo maarufu cha TV Marekani kiitwacho BET ambapo Platnumz amekua na mwaka mwingine mfululizo wa kuwa nominated na sasa ni kwenye tuzo za BET Awards 2016.
Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa >>> ‘Ningependa
niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana
wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa
kwenye tunzo za BET #BETAwards America’
Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa
nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya
kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania huku Beyonce, Rihanna na Drake wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.
Tuesday, 24 May 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments