Open top menu
Friday, 27 May 2016
Yanga mabingwa wa shirikisho


Mchezo huu uliopigwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam, ulishudia kikosi cha Yanga, ilipata ushindi wake kupitia kwa magoli ya mshambuliaji Amisi Tambwe aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya tisa ya kipindi cha kwanza kisha akaongeza bao la pili katika dakika ya 47 ya kipindi cha pili .

Katika dakika ya 81 winga Deus Kaseke, alihitimisha kazi kwa kufunga bao la tatu baada ya kuunganisha krosi ya Simon Msuva.Bao la kufutia machozi la Azam,liliwekwa kambani na mshambuliaji Didier Kavumbagu.

Licha ya Yanga kushinda mchezo huu wa fainali Azam ndio wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la shirikisho huku Yanga wakiwakilisha katika michuano ya klabu bingwa Africa.
Read more
Tanzania ina upungufu wa sukari sasa hivi, imebidi Waziri mkuu aongee Bungeni


April 27 2016 Bunge limepitisha bajeti ya Makadilio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017
Katika hotuba ya kuhitimisha bajeti hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa hotuba na moja ya jambo lililowekewa msisitizo ni hii ishu ya kupanda bei kwa bidhaa ya sukari, Waziri Majaliwa hajalikalia kimya na kusema>>’

Ni kweli kwamba uzalishaji wa sukari nchini upo chini ya kiwango cha mahitaji, mahitaji ya sukari ni tani laki 4 na 20 na kiwango cha uzalishaji ni tani laki 3 na 20 hivyo tunaupungufu wa tani laki moja‘ –Waziri Mkuu Majaliwa

Sukari iliyokuwepo kwenye maghala yetu imepungua, lakini tumeshaagiza na ni ile tu ambayo imepungua, hivyo wananchi watambue sukari itaingia muda si mrefu kwa ajili ya mahitaji ya kitaifa‘ – Waziri Mkuu Majaliwa

Natoa maagizo kwa maafisa biashara wote wafanye ufuatiliaji kwenye maduka kuona kuwa sukari haifichwi na kuuzwa kwa bei ya juu, ni matumaini yangu kuwa Watanzania watanunua sukari ileile kwa bei elekezi‘ –Waziri Mkuu Majaliwa

ULIIKOSA RIPOTI YA TUHUMA ZA RUSHWA TANZANIA NA MENGINE YA WAZIRI MKUU AKIWASILISHA BAJETI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI..
Read more
Rais Magufuli kujaza vijana Serikalini, amegudua haya kwa vijana..

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya stori kubwa ni hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Magufuli kujaza vijana Serikalini‘ Gazeti hili limeripoti kuwa Magufuli amesema kuanzia sasa wateule wengi wa Serikali watakuwa vijana kwa kuwa amegundua wengi hawapendi rushwa.

Gazeti hilo limeongeza kauli ya Rais Magufuli kuwa anafahamu kwamba vijana hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka Taifa katika maendeleo anayoyatamani kwani aliowaweka tayari ameshaanza kuona matunda ya kazi zao.

Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa makandarasi wa mikoa ya Dar es salaa, Mbeya na Dodoma.
Read more
JOSE MOURINHO ASAINI KUIFUNDISHA MAN UNITED


Uongozi wa Man United leo May 27 2016 umetangaza rasmi kumpa mkataba wa miaka mitatu, kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho wenye kipengele cha kubaki katika klabu hiyo hadi mwaka 2020.
Jose Mourinho ametangazwa na klabu hiyo lakini atajiunga na kuanza kufanya kazi rasmi msimu wa mwaka 2016/2017 hii ina maana tutaanza kumuona Mourinho akiiongoza Man United  kama kocha mkuu wakati wa mechi za maandalizi ya mechi za msimu.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho alifukuzwa kazi na Chelsea December 2015,  kocha huyo mwenye asili ya Ureno toka mwaka 2003 hadi sasa akiwa kama kocha amefanikiwa kushinda jumla ya Makombe 23 katika nchi 4 tofauti.
Read more
Tuesday, 24 May 2016
Diamond kwenye headlines nyingine na Wizkid, AKA, Drake, Beyonce na Rihanna

May 20 2016 Tanzania imeamka na habari nyingine njema za Diamond Platnumz kuchaguliwa tena kushiriki kwenye tuzo za kituo maarufu cha TV Marekani kiitwacho BET ambapo Platnumz amekua na mwaka mwingine mfululizo wa kuwa nominated na sasa ni kwenye tuzo za BET Awards 2016.

Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa >>> ‘Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET #BETAwards America’

Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania huku Beyonce, Rihanna na Drake wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.
Read more
Makundi ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika yamepangwa, Yanga yupo Kundi A

Baada ya kumalizika kwa hatua ya mtoano ya michezo ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa barani Afrika, leo May 24 2016 shirikisho la soka barani Afrika CAF na ilichezesha droo ya kuzipanga timu hizo zilizosalia katika Makundi mawili ya A na B.

Kwa upande wa Tanzania Yanga ndio inawakilisha Taifa, nafasi ambayo iliipata baada ya kuitoa GD Esperanca ya Angola kwa jumla ya goli 2-1 katika hatua ya 16 bora.
Read more

Followers