Mkuu Wa Chuo Cha MusomaUtalii Ally Nyambi |
Maktaba
kwa ajili ya kujisomea katika chuo cha Musoma Utalii (MUC) inatarajiwa kuanza
kutumika rasmi kuanzia tarehe moja ya mwezi wa nane mwaka huu
Hayo yamebainishwa
na mkuu wa chuo hicho Ally Nyambi siku ya Ijumaa katika mkutano maalumu kati ya
wanachuo na uongozi wa chuo hicho (College baraza) wakati wa kujibu maswali
yanayowatatiza na kuwahusu wanachuo hao
Akijibu
swali la Mgecha Safari Mussa mwanafunzi wa elimu ya awali chuoni hapo aliyetaka
kujua ni lini Maktaba iliyopo chuoni hapo itaanza kutumika, mkuu huyo wa chuo
alieleza kuwa maktaba hiyo itaanza rasmi kutumika mnamo Agosti 1, 2016
“Ni
kweli kabisa mmekuwa mkipata shida pale mnapotaka kujisomea, Uongozi wa chuo
umeliona hilo na kulifanyia kazi, tunayo maktaba ya kisasa kabisa ambayo
imekalika na tunasubiri Tarehe moja ya mwezi ujao ili ianze kutumika” alisema
mkuu huyo wa chuo
Pia
mkuu huyo wa chuo alisisitiza kuwa katika Maktaba hiyo kuna vitabu mbalimbali
ambavyo vitakidhi mahitaji ya wanachuo hao na kuwataka wanachuo hao waanze
kujijengea tabia ya kujisomea
Pamoja
alibainisha kuwa uongozi wa chuo umeandaa kanuni mbalimbali za kufuatwa na
wananchuo ili kuweza kuruhusiwa kutumia Maktaba hiyo huku akisisitiza kuwa
hakuna mwanachuo atakaye ruhusiwa kuingia kujisomea katika maktaba hiyo bila ya
kuwa na vitambulisho
“Pamoja
na kuwa kutumia maktaba ni haki yenu, ila hakuna kitu kinachoenda bila ya kuwa
na utaratibu, hivyo basi kuna kanuni na taratibu ambazo tumezipanga na mta
bandikiwa kwenye ubao wa matangazo mzione, ila mojawapo ni kwamba hakuna
mwanafunzi atakayeingia maktaba bila ya kuwa na kitambulisho” alikaririwa mkuu
huyu wa chuo
Mkutano
baina ya wanachuo katika chuo cha Musoma Utalii - Tabora na uongozi wa chuo
hicho ulifanyika ijumaa ya Julai 16, 2016 katika ukumbi wa Nyerere chuoni hapo
0 comments